MADAKTARI nchini wametakiwa kufanya mikutano ya kijamii na wananchi ili kuwapa fursa ya kujua magonjwa yanayo wakabili.
Hayo yalielezwa na Dk. Manase Frank
pichani wakati akitoa mada katika kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya
ya Jamii Tanzania (TPHA) lililofanyika Hoteli ya Kebby Mwenge jijini
Dar es Salaam leo asubuhi.
"Changamoto kubwa tuliyonayo ni wananchi
wengi kutojua magonjwa yanayowasumbua hivyo ni muhimu kwa madakatari
kuitisha mikutano itakayowakutanisha na wananchi ili kuondoa changamoto
hiyo" alisema Dk. Frank.
Alisema wagonjwa wengi wamekuwa wakikata
tamaa kwa kuchangiwa na kauli za baadhi ya madaktari ambao wanashindwa
kujua tatizo la mgonjwa husika hivyo wakati umefika wa madaktari
kushirikiana kwa karibu na jamii, viongozi wa dini ili kuondoa
changamoto hiyo.
Akitolea mfano wa kijana mmoja ambaye
alifiwa na ndugu zake wote wa karibu kutokana na ugonjwa wa ukimwi na
kuishi kwa kunyanyapaliwa lakini baadaye afya yake ilikuja kuimarika
kufuatia ushauri uliotolewa na daktari kwa jamii iliyokuwa ikimzunguka
wakati wa ugonjwa wake.
Mtoa mada mwingine Profesa Andrew Swai aliomba serikali wakati wa siku ya Jumamosi na Jumapili kufunga baadhi
ya barabara ili zitumike kwa wananchi kufanya mazoezi ya kutembea ili
kujenga afya za miili yako na kuepukana na magonjwa kama kisukari.
Akizungumzia changamoto ya matumizi ya bodaboda Dk.Chilolo
Edward (wakatikati) alisema kwa mwaka jana katika Hospitali za mikoa ya Morogoro,
Tumbi Pwani na Shinyanga kulikuwa na ajali 895 huku majeruhi wakiwa
4813.
Alisema majeruhi waliolazwa katika
hospitali hizo walikuwa ni 4525, waliopewa rufaa kwenda hospitali za
Bugando na Muhimbili walikuwa 71 na waliolazwa ni 702.
Alisema vifo vilikuwa 81 hivyo vilitokea baada ya kufikishwa Hospitalini ni 70 na vilivyotokea eneo la ajali vilikuwa 11.
No comments:
Post a Comment