Akielezea katika kongamano hilo, Afisa wa TPHA ambaye pia ni msimamizi na mtaafiti wa masuala ya kupambana na madhara ya Tumbaku, Dk. Bertha Maegga amebainisha kuwa, kwa sasa Chama hicho kinaendesha mradi uliopewa jina la “80 CHILDREN STRONG” ukitoa elimu kwa vijana wadogo wenye umri wa miaka 10-14, hasa wa shule za msingi.
Dk. Maegga akihutubia umati wa wanafunzi wa shule hizo saba katika kongamano hilo lililofanyika shule ya Msingi Kijitonyama Visiwani, aliwataka wazazi, walimu, walezi na jamii kuwalinda na kukemea watoto wao kuachana na vitendo vya matumizi ya bidhaa za Tumbaku ikiwemo sigara, ugoro, shisha na Tumbaku yenyewe.
Aidha, amebainisha kuwa, wameweza kulenga kundi hilo kutokana na kuwa na changamoto za kiukuaji wa kiakili na kisaikolojia.
“Umri huu kuna utundu na utukutu mwingi na akili nazo bado hazijakomaa kuepuka ushawishi wa namna mbalimbali ukiwemo na wa matendo yasiyofaa katika maisha yao ya baadaye.
Tukiweza kuwalinda katika umri huo. watabaki salama hadi watakapojitambjua nafsi zao na kuamua mambo ya busara na salama katika maisha yao ya baadae” alibainisha Dk. Maegga.
Kwa
upande wake, Dk. Ali Mzige mganga wa hospitali ya kimataifa ya
Afya ya uzazi ametoa elimu kwa vijana hao na kubainisha kuwa sigara,
tumbaku, shisha, ugoro na kuberi ni hatari kwa afya za mwili huku
ikisababisha magonjwa mbalimbali.
Miongoni mwa magonjwa hayo yatokanayo
na matumizi ya sigara ambapo wanaoathirika zaidi ni vijana kwa sababu
ya kufuata mkumbo pamoja na kuhisi kwamba uvutaji wa sigara unaongeza
sifa ya kuwa mwanaume kamili kitu ambacho si kweli.Bofya hapa kwa maelezo zaidi
No comments:
Post a Comment