![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgu-mYU5UiZckqal4yzMBz6jDEIFJaEI0Mf8TloOPFmEl2v1UJlZQeQqMxcYA1JU0QGIMhC3TG1KvoRzPYmyY1A1fPr-MLbuk-uD-rJzL1HL1-yyV6V1WQYaPVpoP3F015PWjBzRg2_NS4/s320/pic%252Bmarufuku-sigara.jpg)
Moshi wa sigara unadaiwa kuingia kwenye vyumba vya
mahakama na kusababisha Jaji Mfawidhi, Aishiel Sumari, mawakili na
karani wa mahakama kuanza kukohoa mfululizo.
Hili linaweza kuwa tukio la kwanza kwa mhimili wa
Dola kutumia mamlaka yake kuzuia uvutaji wa sigara kwenye maeneo ya wazi
ya umma licha ya Sheria inayosimamizi bidhaa za tumbaku ya mwaka 2003
kuharamisha.
Tukio hilo limekuja miezi minne tangu Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid kutoa agizo la kuzuia uvutaji wa
sigara hadharani ikiwamo katika ofisi za umma.
Kwa mujibu wa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu,
Benard Mpepo, Marealle aliwekwa mahabusu iliyopo mahakamani hapo kuanzia
saa tano asubuhi hadi saa nane mchana.
Mpepo alisema Marealle aliwekwa mahabusi kwa kosa
la kuidharau mahakama chini ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu kifungu 114
kama ilivyofanyiwa marekebisho na Bunge mwaka 2002.
Naibu Msajili alisema kifungu cha 114(b) cha
kanuni ya adhabu kama kilivyofanyiwa marejeo na Bunge mwaka 2002
kinakataza mtu kufanya matendo yatakayoharibu usikilizaji wa kesi.
Mpepo alisema adhabu ya kosa hilo ni kifungo cha
miezi sita jela au kulipa faini ya Sh500, lakini ilionekana adhabu ya
kukaa mahabusi kwa muda huo inatosha kuwa fundisho kwake.
Machi 12, mwaka huu, Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii iliamua kuchukua hatua mahususi katika kuzuia matumizi ya bidhaa
za tumbaku katika maeneo ya umma nchini kote.
Dk Rashid alisema madhumuni ya agizo hilo ni
kuilinda jamii kutokana na madhara yatokanayo na moshi wa sigara ambao
wataalamu wanasema unaweza kusababisha ugonjwa wa saratani.
Agizo hilo la Waziri wa Afya lilihusu maeneo yote
ya umma ambayo yanajumuisha ofisi zote za Serikali na taasisi zake, watu
binafsi, vyuo na kwenye mikutano na shughuli za umma.
Maeneo mengine ni vituo vya huduma za afya ikiwamo
hospitali, vituo vya afya na zahanati, vituo vyote vya usafiri, sehemu
za mikutano, bustanini na kwenye fukwe.CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment