Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime,
jana alithibitisha kutokea kwa ajili hiyo ya Dodoma, saa 3:45 usiku,
katika eneo la Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Alisema basi hilo lilikuwa likitokea Mwanza kwenda
Morogoro liligongana na gari ndogo aina ya Toyota Mark II iliyokuwa
likiingia barabara kuu kutokea Nzuguni.
“Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo
kuingia barabarani bila kuwa makini na kusababusha kushindwa kumpa
kipaumbele aliyekuwa barabara kuu kupita kwanza.
“Lakini pamoja na makosa ya gari ndogo, suala la mwendo kasi wa dereva wa basi umesababisha madhara kuwa makubwa,” alisema.
Aliwataja waliopoteza maisha ambao wote ni
waliokuwa katika gari ndogo kuwa ni Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ),
Monduli mkoani Arusha, Jackson Lazaro aliyekuwa dereva wa gari dogo.
Wengine waliofariki katika ajali hiyo ni Mkazi wa
Makole, Helena Chiuyo (36), Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule
ya Sekondari ya City ya mjini hapa, Fatuma Mtauga (17) na Mkazi wa
Kisasa Stella Giseon (36).
“Dereva wa gari dogo alikuwa akitokea kijiji
Nzuguni kuingia barabara kuu ya Dodoma kuelekea Morogoro kugongana basi
ambalo lilipoteza mwelekeo na kuingia porini umbali usiopungua mita 300
na kugonga mti na kisha kusimama,”alisema Kamanda Misime.
Alisema dereva wa basi ambaye ni Mkazi wa Kirumba Mwanza, Leonard Magesa (51) anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Naye Ofisa Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya
Rufaa ya Dodoma, Cecilia Sanya, alisema alipokea majeruhi huyo saa 6.20
Fatuma Patrick kutoka eneo la ajali akiwa majeraha sehemu mbalimbali za
mwili ikiwemo kichwani .
“Waliongoza na wauguzi wa zamu kwenda katika eneo
la tukio wakiwa na gari la wagonjwa, walivyofika pale walikuta watu hao
wamefariki dunia,” alisema Cecilia.
Naye mmoja wa mashuhuda, Christian Kihonda,
alisema dereva wa basi alikuwa katika mwendo kasi baada ya mgomo
kumalizika juzi mchana.kwa habari zaidi
No comments:
Post a Comment