![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjiOb5VaCo7PXP9FMHMPSzjXO0HRCDaxypN3nBBlD7wy0PDqRRapo7-bjZEgzOhcHkQ0SmfzyP7kkcxfdxDzGl4qqEUiMeSJKt-4SFe8fuXXvRAXzjr_e_i10DPHR0p2YTJlqaYrWz3ubw/s1600/mtoto_baraka.jpg)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi
alisema juzi mjini hapa kwamba kiganja hicho kilipatikana kutoka kwa
mkazi wa Kijiji cha Malonje, Sajenti Kalinga (54) ambaye anafanya kazi
ya useremala.
Alisema awali, polisi walimkamata mganga wa kupiga
ramli aliyemtaja kwa jina la Gunela Shinji wa Kijiji cha Kipeta kuwa
ndiye aliyehusika kukata kiganja hicho.
Alisema baada ya kumbana mganga huyo alimtaja
Kalinga kwamba ndiye aliyemtuma kuleta kiganja hicho cha mtu mwenye
ulemavu wa ngozi (albino).
“Tulimbana mtuhumiwa akatueleza kuwa aliyemtuma kiganja hicho ni Sajenti Kalinga kwa dau la Sh100 milioni,” alisema Msangi.
Kamanda Msangi alisema mtuhumiwa Shinji aliwapeleka polisi hadi kwa mteja wake huyo na kufanikiwa kumkamata.
“Polisi walifika nyumbani kwa mtuhumiwa Kalinga na walipomhoji kwa kina, alikitoa kiganja hicho na kuwakabidhi.”
Alisema hadi juzi, watu sita walikuwa
wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo wakiwamo waliokamatwa
mwaka jana na wengine mwaka huu.
Wanaoshikiliwa ni baba wa mtoto huyo, Cosmas Lusambo, mganga wa jadi, Miambo Kameta; Shinji na Kalinga.
Mtoto Baraka Cosmas aliyekatwa kiganja hicho
amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya akiendelea na matibabu chini ya
uangalizi wa mama yake Prisca Shaaban (28) ambaye sasa ana watoto
watano, wanne kati yao wakiwa albino.
Mama huyo alisema amepata taarifa za kukamatwa kwa
watuhumiwa hao na kwamba ingawa hajui masuala ya kisheria, anaamini
Serikali itachukua hatua stahiki kwa watakaobainika kuhusika.
Msangi alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mkoani Rukwa wakati wowote.Kwa Habari Zaidi
No comments:
Post a Comment