Wednesday, 8 April 2015

Mambo 10 ya kujiokoa na shambulio la ugaidi

Wakati mashambulizi ya kigaidi yakiendelea kutikisa maeneo mbalimbali duniani ikiwamo nchi jirani ya Kenya huku kukiwa na angalizo kuwa huenda na Tanzania ikashambuliwa, jarida moja la kimataifa limetaja mambo 10 ya kufanya baada ya shambulio.

Mambo hayo ambayo ni hatua za kumsaidia mtu aliyenusurika katika shambulio husika ili kunusuru maisha yake, yametajwa wakati zikiwapo taarifa za tisho la shambulizi katika miji ya Dar es Salaam na Mwanza.
Jarida hilo lilifanya mahojiano na wataalamu wa sayansi ambao walitoa mapendekezo ambayo mtu anaweza kufuata  wakati au baada ya mlipuko na kuwa asilimia 50 ya watu wanaokutwa katika mashambulizi ya kigaidi  hujeruhiwa na wengine kupoteza maisha kwa sababu hawafahamu jinsi ya kujihami.
Tanzania iliwahi kukumbwa na shambulio la ugaidi mwaka 1998 wakati Ubalozi za Marekani, jijini Dar es Salaam ulipolipuliwa na kusababisha vifo vya watu kumi na moja. Shambulio hilo lilitokea sambamba na lile la ubalozi wa nchi hiyo, Nairobi, Kenya lililosababisha vifo ya watu 213.
Uvumi zaidi umeendelea kuenea baada ya shambulio la kigaidi lililotokea wiki iliyopita katika Chuo Kikuu cha Garissa, Kenya na kuua  wanafunzi 148.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe alisema pamoja na kusikia taarifa hizo, mpaka sasa Serikali haijaweza kuthibitisha ripoti hizo zinazoenea, lakini inachukua tahadhari juu ya suala hilo.Kwa Habari Zaidi

No comments:

Post a Comment