
Kushushwa kwa mtoto huyo kumekuja baada ya Umoja
wa Vijana wa Chama cha Wananchi (CUF) Manispaa ya Mtwara Mikindani,
kumtembelea Lipunga kwa lengo la kumjengea nyumba imara kutokana na
kuishi katika mazingira hatarishi.
“Nilipoona mvua zinanyesha nikaona bora nimnusuru
mjukuu wangu asisombwe na mafuriko kwa vile sina nguvu za kuweza
kumpandisha na kumteremsha mara kwa mara,” alisema Lipuga na kuongeza:
“Mjukuu wangu ni mlemavu hawezi hata kukaa, katika
kipindi chote hicho amekuwa akilala tu, najua anateseka sana hasa
ukizingatia umbali wa dari na paa la bati ni karibu sana wakati wa jua
kali anaumia sana ila sina jinsi.”
Alisema baba wa mtoto huyo ambaye ni mwanaye hajulikani alipo na kwamba jukumu la kumlea limeachwa mikononi mwake bila msaada.
Mjumbe wa umoja huo, Mwanahamisi Hamisi alisema
chama chake kimeguswa na hali hiyo, hivyo kimeamua kumuondoa katika
nyumba yenye miundombinu duni.
“Milango ipo wazi kwa wadau wengine kumsaidia bibi
huyu ili aweze kuishi vizuri na mjukuu wake...inatia huruma yule mtoto
anaathirika sana na jua kali kule darini, anahitaji kusaidiwa,” alisema
Mwanahamisi.
Hata hivyo, wakati huo, manispaa hiyo ilikumbwa na mafuriko Januari mwaka huu.
Zaidi ya nyumba 200 zilizingirwa na maji kusababisha hasara kwa wananchi ikiwamo kuharibika mali zao zikiwamo nguo na vyakula.
Katika janga hilo, hakuna mtu aliyeripotiwa kupoteza maisha.CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment