BAADHI ya waganga wa kienyeji nchini sasa wamegeuza matatizo ya
Watanzania kuwa mitaji yao ya kujipatia mamilioni ya fedha kwa madai
kwamba wanawapatia tiba.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi
Jumamosi umebaini kuwa wengi wa waganga hao wanaojipatia fedha kwa njia
ya kuwadaganya wananchi ni wale ambao hawajasajiliwa na Serikali. Moja
ya uthibitisho wa kwamba huduma hiyo haramu huwapatia fedha nyingi
waganga hao ni kuenea kwa mabango mengi yanayotangaza kuwepo kwa waganga
hao.
Katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam na miji
migine mikubwa nchini huwezi kutembea mwendo mrefu bila kukutana na
kibao kinamtangaza mganga wa kienyeji kutoka ndani na nje ya nchi.
Miongoni
mwa waganga hao, wapo wanaojitangaza kutibu watu walio na matatizo ya
nguvu za kiume, wanaotaka kupata utajiri wa haraka, kutibu mwanafunzi
ambaye hana akili darasani, kuolewa au kuoa haraka, kumvuta mpenzi aliye
mbali, kunenepesha makalio na kurefusha maumbile ya sehemu za siri kwa
wanaume na mengineyo.Bofya hapa kwa habari zaidi
No comments:
Post a Comment