Idadi ya watu imeongezeka mara mbili toka watu milioni 25 mwaka
1990 hadi watu milioni 45 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012. Hali hii,
inaleta changamoto kubwa katika utoaji wa huduma bora za afya , huduma
za kijamii kama vile maji na elimu hasa kwa kuzingatia kuwa, asilimia 70
ya watanzania vijijini na karibu asilimia 30 ya wanawake walio kwenye
umri wa kuzaa hawana elimu.
Mbio hizo za kiuchumi , zinaweza kufanikiwa tu iwapo kutakuwa na
uwiano wa huduma muhimu na za msingi ikiwemo zile za afya hasa ya uzazi,
kwa akina mama,watoto wachanga na watoto chini ya umri wa miaka mitano
kufikia mwaka 2035.
Mafanikio hayo, yanatakiwa kwenda sambamba na kasi ya kupunguza
kama si kuondoa kabisa vifo vya watanzania hasa akina mama,watoto
wachanga, watoto chini ya miaka mitano na watoto waliozaliwa wafu kwa
zaidi ya asilimia 80. Hii ina maana ya kuokoa maisha ya watu 60,000 kwa
mwaka.
Tafiti na takwimu mbalimbali zinaonyesha kuwa, takriban wanawake
7,900 wa Tanzania hufa kutokana na matatizo ya ujauzito na kujifungua.
Watoto 40,000 hufariki katika kipindi cha siku 28 za mwanzo wa maisha
yao huku wengine takriban watoto 100,000 hupoteza maisha kabla ya kufika
umri wa miaka mitano.Kwa Maelezo zaidi
No comments:
Post a Comment