"Siku hiyo sintaisahau maishani, iliyonifanya nilazimike kuacha
ukeketaji…majira hayo ya alfajiri nilikeketa wasichana 20, watano kati
yao waliishiwa nguvu kabisa kwa kutokwa damu nyingi na
kuzirai…nilichanganyikiwa sikujua nifanye nini. Mume wangu aliiangalia
hali hiyo akaniambia shauri yako utafungwa na serikali…Niliogopa
sana…sikujua la kufanya. Baadaye wasichana wale walipata fahamu …nikaapa
kuwa sitafanya tena ukeketaji" anasema ngariba mstaafu Mariana Ndama,
66, mkazi wa kijiji cha Ikungi mkoani Dodoma.
Kwa Mariana, tukio hilo alilichukulia kuwa sio la kawaida kabisa
hata kudhani kuwa, amechezewa (kurogwa ) na maadui zake wasiomtakia mema
kwa mafanikio na umaarufu aliokuwa anaupata kwa ukeketaji wasichana.
Bofya hapa kwa stori zaidi
No comments:
Post a Comment