Thursday, 19 March 2015

Uhaba wa Damu waikumba Hospitali ya Rufaa Iringa

Hospitali ya Rufaa Mkoani Iringa imeshindwa kuwahudumia wagonjwa wa upungufu wa damu kutokana na kukabiliwa na upungufu wa damu hospitalini hapo.

Mtekinolojia wa maabara ya hospitali ya rufaa wa mkoa Iringa Bw. Amulike Mwalongo amesema, hali hiyo imetokana na wananchi kukosa kuchangia damu, ukosefu wa vifaa vya kutolea damu na ukosefu wa fedha.

Bw. Mwalongo amesema, tokea Disemba mwaka jana hospitali hiyo haijapata damu kutoka benki ya damu ya mkoani Mbeya kwani hakuna damu ya kutosha.

Naye Afisa ubora wa viwango vya maabara Bibi Emmy Mkupasya amesema, ukosefu wa uelewa wa wananchi juu ya uchangiaji wa damu kumepelekea kuiachia serikali kwa imani ndiyo yenye jukumu hilo.Kwa Habari Zaidi

No comments:

Post a Comment