Hata hivyo, gazeti hili lilishindwa kufanya
mahojiano na muuguzi huyo jana kwa kuwa alikuwa akihojiwa katika Kituo
cha Polisi cha Oysterbay, kuanzia saa nne asubuhi hadi mwandishi
alipoondoka kituoni hapo saa 11 jioni.
Kwa mujibu wa shangazi yake Pili, Fatuma Mbasa,
muuguzi huyo alirudi nyumbani saa 10 alfajiri jana akiwa katika hali ya
kulewa na makovu kadhaa shingoni.
“Inaonekana walimpa dawa za kulevya kwa sababu
alikuwa kama teja, hajiwezi na ana majeraha kadhaa na alikuwa
akilalamika kuwa na maumivu shingoni,” alisema Mbasa.Soma Zaidi
No comments:
Post a Comment