Friday, 20 March 2015

Tahadhari ya ugonjwa wa dengi ifanyiwe kazi

Zipo taarifa kuwa jiji la Dar es Salaam linaweza kukumbwa na mlipuko mwingine wa ugonjwa wa dengi kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kukithiri kwa uchafu, hasa maji yaliyotuwama kwenye madimbwi na pia kwenye makopo, matairi ya magari na aina nyingine za taka ngumu.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr), ugonjwa huo hauna tiba wala chanjo na kwamba, tafiti mbalimbali zimebainisha kuwa njia pekee ya kuepuka madhara yake ni kuimarisha usafi wa mazingira.
 
Taarifa hiyo ambayo ni miongoni mwa zile zilizokuwamo kwenye gazeti hili jana ilieleza kuwa mazalia ya mbu aina ya Aedes aegypti, ambaye ndiye anayeeneza ugonjwa wa dengi, mara nyingi huwa ni kwenye makopo ya plastiki na matairi ya magari yaliyotupwa hovyo. Katika utafiti ulifanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Mei hadi Julai mwaka jana, imebainika kuwa vyombo vinavyoruhusu maji kutuwama vinaashiria kuwapo kwa hatari ya mlipuko wa dengi na hali hiyo ipo katika wilaya zote za Dar es Salaam, kwa maana ya Kinondoni, Ilala na Temeke.Kwa habari zaidi
 

No comments:

Post a Comment