Friday, 20 March 2015

Vituo vya afya viimarishwe kupunguza msongamano wa wagonjwa hospitalini.

Kuna taarifa kuwa Hospitali ya Rufaa ya Temeke iliyopo katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam inakabiliwa na msongamano mkubwa wa wagonjwa kiasi cha kushindwa kuwapatia vifaa muhimu wagonjwa wanaolazwa kama shuka za kulalia na vitanda.
 
Taarifa zilizoripotiwa jana na gazeti hili zikimkariri mganga mkuu wa hospitali hiyo zilionyesha kuwa hali ni mbaya na kwamba jitihada za haraka zinahitajika sasa ili kupunguza changamoto zitokanazo na mrundikano wa wagonjwa hospitalini hapo.
 
Inaelezwa kuwa hivi sasa, idadi ya shuka zilizopo katika hospitali hiyo ni 1,200 wakati mahitaji halisi yatokanayo na idadi kubwa ya wagonjwa wanaofikishwa na kulazwa hapo kila uchao ni zaidi ya shuka 2,400.
 
Hili ni tatizo kubwa. Ukweli huu unatokana na ukweli kwamba uwiano wa shuka zilizopo na wastani wa zile zinazohitajika hauko sawa. Ni kwa sababu uhaba uliopo unafikia takriban nusu ya shuka zinazohitajika na hali hiyo siyo nzuri hata kidogo. Bofya hapa kwa habari zaidi

No comments:

Post a Comment