Sunday, 8 March 2015

Wakorea wahaha kukwepa kufungiwa

Raia wa Korea Kaskazini wanaofanya biashara ya dawa za tiba asili na tiba mbadala, wanaweka mazingira bora ya kuihadaa serikali isifanikiwe kufunga vituo vinavyouza dawa hizo kinyume cha taratibu.

Taarifa za kuwapo kwa vituo hivyo zilifichuliwa na gazeti la Nipashe takribani wiki tatu zilizopita, ambapo miongoni mwa kasoro zilizoripotiwa, ingawa kwa kukanushwa na wamiliki wake, ni pamoja na dawa hizo kudaiwa kuwa na kiwango kikubwa cha madini chuma.

Pia, dawa hizo zilikuwa zinatolewa kwa Watanzania pasipokuwa na jina, aina ya miti iliyotumika kuzitengeneza ama namna zinavyotibu magonjwa husika.Endelea kusoma

No comments:

Post a Comment