Friday, 27 March 2015

Vyakula vinavyoimarisha nguvu za kiume


Kula nafaka zisizokobolewa kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri kiafya zina saidia kutokupa mwili wa mafuta mengi, ikumbukwe uwapo wa mafuta mabaya yanaharibu mishipa ya damu ikiwamo ya uume.
Tangawizi ni aina ya kiungo mizizi ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Mzunguko unapokuwa mzuri huwezesha damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi ikiwamo uume.
Tangawizi imekuwa ikitumika sana maeneo ya Asia kwa ajili ya wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume.
Viungo ambavyo viko katika pilau ni mojawapo ya vitu ambavyo miaka na miaka imetumika maeneo ya Asia na Amerika ya Kaskazini kama viungo vyakula vinavyoimarisha nguvu za kiume.

Mchanganyiko wa mbegu mbalimbali za matunda ikiwamo tikiti maji, mbegu za maboga husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya njema.
Vanila husaidia kuamsha hamasa mwilini, vanila ni aina ya kirurubisho ambacho huwamo ndani ya vyakula ikiwamo ice cream.
Asali ina madini yanayoitwa boron ambayo husaidia mwili kutumia homoni.
Hata vitabu vya dini hueleza ulaji wa asali na masega yake kama mlo wenye kuupa mwili nguvu. Zipo tafiti lukuki kuhusu faida za asali ikiwamo ya kuongeza nguvu za kiume.
Karanga huhusika moja kwa moja na kutunza mfumo wa mzunguko wa damu kuwa na afya. Husaidia kuimarisha mzunguko wa damu katika maeneo ya uzazi hivyo kuongeza msisimko wa tendo.
Pia karanga zina madini muhimu kama vile madini ya magineziamu, tindikali ya foliki na madini ya zinki ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa mbegu za mwanaume na kuongeza hisia.
Ulaji wa Chokoleti huongeza uchangamfu mwilini hivyo kumuwezesha mtu anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na mguso sahihi kwenye fikra zake.
Chocolate ina phenylethylamine kemikali ambayo husababisha hisia za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume kufika kileleni. Pia choklate ina kiasi kikubwa cha nishati inayokupa nguvu mwilini.
Vyakula vingine ni pamoja na pilipili manga, abdalasini, figs, makoma manga, kweme na njugu mawe.Endelea

No comments:

Post a Comment