
Nyuzinyuzi kwa kitaalamu dietary fibers
zinapatikana kwa asili katika vyakula tunavyokula vinavyotokana na
mimea. Hii ni sehemu ya vyakula vya mimea ambayo tumbo la mwanadamu
haliwezi kusaga, kwa hiyo inatoka kwa kupitia haja kubwa kama kinyesi.
Kuna aina mbili za nyuzinyuzi, inayoyeyuka na
isiyoyeyuka katika maji. Aina zote mbili ni muhimu kwa afya ya binadamu
kwa kusaidia usagaji wa chakula, kuzuwia magonjwa ya moyo, kisukari,
uzito kupita kiasi, saratani ya utumbo mpana na kukosa choo kikubwa.
Nyuzinyuzi zinaondoa sumu na uchafu kutoka tumboni, zinasafisha tumbo na ni chakula cha bakteria wazuri wanaoishi tumboni.
Nyuzinyuzi zinazoyeyuka zinanyonya maji na
kutengeneza kitu laini tumboni ambacho kinapunguza kasi ya usagaji
chakula tumboni. Ndiyo kusema, nyuzinyuzi zinazoyeyuka zinamfanya tumbo
kubaki na chakula kwa muda mrefu. Mlaji anaepuka kula mara kwa mara na
hata kuwa na uzito kupita kiasi.
Kupunguza kasi ya kusaga chakula tumboni pia, kuna
saidia kupunguza wingi wa sukari katika damu. Kwa hiyo dawa ya insulini
inayozalishwa mwilini ili kupunguza wingi wa sukari katika damu,
itaendelea kufanya kazi vizuri na kumwepusha mtu na ugonjwa wa kisukari.
Vilevile, nyuzinyuzi zinazoyeyuka zinaufanya
utumbo kunyonya kiasi kidogo cha mafuta aina ya lehemu yanayotokana na
vyakula. Matokeo yake mwili utakuwa na kiwango kidogo cha aina mbaya ya
lehemu, inayochochea magonjwa ya moyo.
Nyuzinyuzi zinazoyeyuka katika maji zinapatikana
kwa wingi katika maharage, karoti, matango na matunda yakiwemo
machungwa, epo, peasi na strawberries.
Kazi kubwa ya nyuzinyuzi hizi ni kuongeza ukubwa
wa mabaki ya chakula kisichosagwa na kutoka nje kama choo kikubwa kwa
wepesi. Kwa hiyo, zinaondoa tatizo la mtu kukosa choo kikubwa na
kuufanya utumbo kufanya kazi vizuri. Chanzo kizuri cha nyuzinyuzi
zisizoyeyuka ni nafaka zisizokobolewa na mbogamboga.
Mahindi na ngano zisizokobolewa, karanga, mbegu, mchicha, kabichi, vitunguu, nyanya na matunda ya aina mbalimbali.
Wasomaji wazingatie kuwa aina zote mbili ya
nyuzinyuzi ni muhimu kwa afya. Watu wale aina mbalimbali za matunda,
mbogamboga na nafaka zisizokobolewa ili kuzipata aina zote mbili.
Kuna watu wanatumia nyuzinyuzi zilizo tengenezwa
kutokana na mimea. Watumiaji wa aina hiyo ya nyuzinyuzi, wawe wanakunywa
maji mengi kwa kila siku na waombe ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya
mara kwa mara.CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment