Umakini kwa mara nyingine tena umewekwa katika uhitaji wa
wataalamu zaidi na kuboresha miundombinu ndani ya sekta ya utabibu wa
upasuaji wa mfumo wa fahamu.
Hii inakuja baada ya ziara ya hivi karibuni na
timu ya madaktari kutoka Hospitali ya Apollo nchini India. Madaktari
ambao walikuwa nchini kwa lengo la kujenga uhusiano unaoendelea kati ya
hospitali hiyo na Tanzania.
Walipata fursa ya kutembelea taasisi mbalimbali
ikiwa ni pamoja na maboresho ya ujuzi kwa wauguzi ambao walipata mafunzo
kutoka Hospitali ya Apollo.
Matibabu ya magonjwa ya mfumo wa fahamu ni mada nyeti yenye matatizo mbalimbali kama yakifanyika kwa namna isiyo sahihi.
Kuvurugika kwa mishipa ya fahamu ni ugonjwa ambao
unatokea katikati na pembeni ya mfumo wa neva. Ambapo kimuundo, upungufu
wa kemikali au umeme kutokuwa sawa katika ubongo, uti wa mgongo au
mishipa mingine, inaweza kusababisha dalili za aina mbalimbali.
Tanzania kwa sasa kuna madaktari saba wa mfumo wa
fahamu ambao wote kwa sasa ni watendaji katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili. Kutokana na kutokuwapo kwa kumbukumbu sahihi za matatizo ya
mifumo ya neva, hakuna uhakika wa kiwango ambacho tatizo hili
linawakumba Watanzania. Hii ni tofauti na wenzao nchini India.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi ya Mfumo wa
Fahamu wa Hospitali ya Apollo iliyopo Bangalore, India, Profesa Krishna
Kambadoor anasema takwimu za wanaougua India inaweza ikawa sawa na
Tanzania.
Profesa Krishna anasema mlo usio kamili
husababisha matukio ya magonjwa ya kisukari na matatizo yanayoambatana
katika sehemu za mwili ikiwa ni pamoja na kupoteza uwezo wa hisia.
Matatizo haya anasema ni pamoja na kuongezeka
idadi ya magonjwa yanayohusiana na umri mkubwa miongoni mwao, yakiwamo
mishipa ya fahamu na moyo kwa ujumla.
Anasema hospitali za Apollo zinatarajia kuleta
jopo la madaktari wataalamu wa mfumo wa fahamu ili kuisaidia Tanzania
kubaini ukubwa wa tatizo na jinsi ya kukabiliana nalo. “Hii ni hatua
ambayo itatazama utengenezaji wa vituo mtaalamu ambapo itaboresha huduma
na kuongeza wataalamu wa afya hapa nchini,” anasema.
Profesa Krishna anasema hospitali za Apollo
zinatazamia kuleta mapinduzi ya tiba kwa magonjwa ya mfumo wa fahamu.
Anasema anahisi hilo linawezekana kwa sababu miaka 20 iliyopita, India
ilikuwa na mazingira kama yanayoonekana kwa sasa nchini ya kutokuwa na
takwimu sahihi.
“India kama Tanzania ilikuwa katika hali kama hii
miongo mitatu iliyopita na tangu wakati imeingia kutoka Taifa
linaloendelea na kuwa karibu sawa na mataifa yaliyoendelea,” anasisitiza
akifafanua:CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment