Sunday, 8 March 2015

Takwimu usafirishaji dawa za kulevya nchini inatisha.

Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimetoa taarifa ya kustusha kuhusiana na mwenendo wa biashara ya dawa za kulevya nchini. Taarifa hiyo iliyoripotiwa jana na gazeti hili inaonyesha kuwa Tanzania ni kinara kwa usafirishaji wa dawa za kulevya miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki.
Inaelezwa kuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi 2013 peke yake, jumla ya Watanzania 433 walikamatwa na dawa za kulevya katika nchi za China na Brazil. Nchi nyingine ya ukanda huu inayotajwa kuwa juu kwa usafirishaji wa dawa za kulevya ni majirani zetu Kenya, ambao wanaifuatia Tanzania kwa kushika nafasi ya pili.
Taarifa hiyo ya UNIC inaeleza zaidi kuwa mbali na kukamata nafasi ya kwanza kwa kuwa na raia wengi wanaokamatwa na dawa za kulevya ughaibuni, Tanzania pia ina waathirika wengi zaidi wa dawa za kulevya, ambao idadi yao imefikia 2,225. Katika eneo hilo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inatajwa kinara barani Afrika, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni hali ya kukosekana kwa amani na utulivu katika nchi hiyo na hivyo kutoa mwanya kwa biashara hiyo (ya dawa za kulevya) kukosa udhibiti makiniEndelea kusoma

No comments:

Post a Comment