Mkazi mmoja wa Miembe Saba wilayani Kibaha mkoani Pwani
amekamatwa na polisi akituhumiwa kuwabaka watoto wake wawili wadogo kwa
zaidi ya miaka miwili sasa.

Watoto hao mmoja mwenye umri wa miaka 15 anayesoma
darasa la saba na mdogo wake mwenye umri wa miaka 11 aliyeanza kubakwa
akiwa darasa la tatu.
Kwa mujibu wa watoto hao, baba huyo alikuwa
anamuita mmoja wa watoto wake chumbani kwake na kumtaka alale na mdogo
wao wa kiume wakati huo akiwa na mwaka mmoja na binti akipitiwa na
usingizi humvua nguo za ndani na kumwingilia huku akimtaka kukaa kimya
na kuvumilia maumivu.
Mke wa mtuhumiwa huyo, ambaye amekuwa akizimia
mara kwa mara kutokana na kulia baada ya kubaini mchezo huo, alisema
aligundua watoto wake wanabakwa Ijumaa iliyopita baada ya mmoja wa
mabinti zake hao kumweleza kuwa baba yake alikuwa amembaka Machi 19,
mwaka huu.
Alisema kabla ya binti huyo kumweleza hivyo,
alimwomba asimpige kwani kuna kitu anataka amweleze, japo ni kibaya
lakini yeye amechoshwa na kimekuwa kikimuumiza kichwa.
“Alisema kila ninapokwenda katika biashara zangu,
anatamani nisiwe ninawaacha hapo, nikamwahidi sitamfanya kitu ili mradi
aseme ukweli tu,” alisema mama huyo.
Baada ya kuhakikishiwa kulindwa, ndipo binti huyo
aliposimulia jinsi ambavyo baba yake amekuwa akiwafanyia na kuwatishia
wakipiga kelele atawaua.
“Niliposikia mwili ulisisimka na ghafla binti
yangu mwingine naye akatokea akilia na kuniambia, ‘hata mimi baba
ananifanyiaga hivyohivyo kila siku unapokuwa umepeleka mboga sokoni
Kariakoo,” alisema mama huyo.
Mwanamke huyo ameomba sheria ichukue nafasi yake
katika tukio hilo kwa kuwa ni la kinyama na pia wataalamu wa saikolojia
wamsaidie binti yake mdogo wa darasa la tano kwani yeye ameathirika
zaidi.
Daktari aliyewapima watoto hao, ameshauri binti huyo mdogo apate ushauri zaidi ili kurudisha akili yake katika hali ya kawaida.CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment