Kila kukicha kumekuwa na kesi za migogoro ya ardhi, mirathi na
hata kesi za wazazi kuozesha mabinti zao wakiwa na umri mdogo licha ya
suala hilo kupigiwa kelele muda mrefu.
Hiyo ni changamoto inayolikabili taifa, huku
baadhi ya watu wakiliona kuwa ni jambo la kawaida na hulipuuza wakati
wengine wanalikemea.
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Haki za
Binadamu Duniani(Amnesty) iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam hivi
karibuni, Tanzania ni moja ya nchi zinaoongoza kwa matukio ya mimba za
utotoni.
Takwimu zinaonyesha kuwa, kwa siku, watoto 16 wanapachikwa mimba za utotoni.
Kwa mujibu wa wataalamu, hali hiyo imekuwa
ikiendelea kwa muda mrefu na kwa asilimia kubwa inazorotesha maendeleo
ya mtoto wa kike.
Ili kumwokoa mtoto wa kike kutoka janga hilo,
jitihada mbalimbali zimefanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali
kuhakikisha inawaokoa hasa wale ambao tayari wameshatumbukia katika
dimbwi hilo.
Utafiti uliofanywa hivi karibuni na Chama
chaWaandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), unaonyesha kuwa katika kipindi
cha mwaka 2012/2013, matukio 228 ya mimba na matukio 42 ya ndoa za
utotoni yaliripotiwa.
Hata hivyo, mimba na ndoa za utotoni zimetajwa
kuwa miongoni mwa vikwazo vinavyowapata watoto wa kike wa Tanzania,
tatizo ambalo bado ni kubwa katika baadhi ya maeneo ya Tanzania Bara na
Visiwani.
Mimba za utotoni na ukatili
Kwa kiasi kikubwa tatizo hilo linakwenda sanjari
na ukatili wa kijinsia ambapo kwa Tanzania Visiwani hali hiyo imeonekana
zaidi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Wilaya ya Kati Unguja, huku upande
wa Tanzania Bara maeneo yenye ukatili dhidi ya wanawake pamoja na mimba
za utotoni yakitajwa kuwa ni Wilaya za Kahama, Tarime, Sengerema,
Newala, Mbulu, Bunda, Nkasi, Babati, Chunya, Dodoma, Bariadi, Busega na
Singida vijijini.
Bokhe Odhiambo (31), mkazi wa Tarime mkoani Mara,
anasema kuwa vitendo vya ukatilli dhidi ya wanawake ndani ya ndoa na
mimba za utotoni kwa watoto wa kike ni mambo ya kawaida na jamii
inaonekana kuwa haina muda wa kuyakemea.
“Kupigwa au kufanyiwa vitendo vya ukatili dhidi ya
wanawake ndani ya ndoa, migogoro ya ardhi na mimba za utotoni kwa
watoto wa kike ni mambo ya kawaida tu kwenye jamii yetu licha ya
wasaidizi wa kisheria kutoa elimu,” anssema Odhiambo.Kwa habari zaidi
No comments:
Post a Comment