Monday, 2 March 2015

Watanzania wapata habari kuhusu Ebola kupitia simu za mkononi



Nchini Tanzania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto
UNICEF limezindua kampeni ya kuhamasisha jamii kuhusu Ebola kupitia
ujumbe wa simu za mkononi kwa ushirikiano na wizara ya afya na kampuni
ya Push Mobile.


Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro
Rodriguez ameiambia Idhaa hii kuwa hata kama mlipuko wa Ebola unaanza
kudhibitiwa Afrika ya Magharibi, bado mtu mmoja akisafiri na ugonjwa huu
anaweza kuhatarisha jamii nzima. Watanzania wapata habari kuhusu Ebola kupitia simu za mkononi | Idhaa ya Redio ya UM

No comments:

Post a Comment