Wednesday, 25 March 2015
Ndoa za utotoni zimekuwa donda ndugu Afrika
TANZANIA ni miongozi mwa nchi za Afrika zenye idadi kubwa ya ndoa za utotoni, hali inayosababisha mtoto wa kike kutokuwa na maendeleo.
Mkoa wa Shinyanga ulio kaskazini magharibi mwa Tanzania ndiyo unaotajwa kuongoza kwa mimba na ndoa za utotoni, ikilinganishwa na mikoa mingine.
Hali hiyo inasababishwa na mambo mengi yaliyowazunguka, jambo ambalo linamfanya mtoto wa kike kuishi katika mazingira magumu.
Mimba za utotoni zimekuwa zikiwatesa watoto katika baadhi ya mikoa kutokana na watu kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na malezi ya watoto na haki zao.
Ili kutokomeza ndoa hizi ni lazima watu wakaungana kwa pamoja kupiga vita ukatili huo, kwani mtoto wa kike ana haki ya kusoma.
Baadhi ya mila, desturi na sheria zinasababisha kuchangia ndoa za utotoni kuongezeka kwa kasi kubwa, hali itakayomfanya mtoto huyo kuwa mnyonge.
Vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti matukio ya kikatili kwa watoto kwa uwazi na ukweli, hali inayofanya mtoto kuona kuwa anajaliwa.
Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef) zinaonesha kuwa, kwa siku moja, watoto 16 wanapata mimba za utotoni.
Hayo yanasemwa na Mkurugenzi Mtendaji Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), Valerie Msoka, baada ya kupokea tuzo ya CEFM Champion kutoka kwa Balozi wa Canada nchini, Alexandre Leveque kuwa balozi wa kupinga ndoa za utotoni na ukeketaji.
Msoka amekuwa mtu wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo, baada ya kuonekana kuwa yeye ndiye anayefaha kuoneza elimu ya kutokomeza ukatili huo kutokana na uhodari wake wa kupigania haki.
“Tuzo hii ni yetu wote, kama si kwa ushirikiano wenu wadau wa maendeleo, vyombo vya habari ambavyo tumefanya kazi kwa karibu na jamii kwa ujumla. Ni matumaini yangu kuwa tutaendelea kushikamana kuhakikisha kuwa hadhi ya mtoto wa kike inalindwa ipasavyo,” anasema.Soma Zaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment